Ili kupakua faili za BRF kwa kutumia kompyuta au kirekodi madokezo cha Braille, tafadhali fuata hatua za hapo chini. Tafadhali zingatia kuwa hatua hizi hazifanyi kazi unapotumia tableti au simutamba ili kupakua faili za BRF.

  1. Ingia ndani kwenye akaunti yako

  2. Tafuta kitabu kwa kutumia kisanduku cha utafutaji

  3. Chagua kichwa cha kitabu

  4. Chagua BRF kutoka kwenye kisanduku cha kushukisha chini (cha mseto) chenye umbizo la upakuaji, kisha bofya kitufe cha upakuaji

  5. Ukiulizwa kama ungependa Kufungua au Kuhifadhi faili, tafadhali chagua Kuhifadhi, kisha chagua eneo ambapo unaweza kuipata kwa urahisi

Dokezo: Vivinjari vingi vya mtandao vinahifadhi faili kwenye folda ya Vipakuzi kimsingi.

Audience
Mwanachama
Help Topics
Mwanachama - Kupakua na Kusoma Vitabu