Ili kuweka upya nenosiri lako, nenda kwenye: Nimesahau nenosiri na ingiza anwani yako ya nenosiri. Utatumiwa baruapepe yenye kiungo cha kuunda nenosiri jipya.

Tazama makala kamili ya msaada

Watumiaji wanaweza kusoma umbizo letu la EPUB kwenye kompyuta zao za Apple na vifaa vya simu vya iOS (kama vile iPhone) kwa kutumia iBooks. 

 1. Ingia ndani kwenye akaunti yako.

 2. Tafuta kitabu kwa kutumia kisanduku cha utafutaji kilichoko kwenye sehemu ya juu ya ukurasa.

 3. Baada ya kukipata kitabu kwenye matokeo ya utafutaji, chagua EPUB kutoka kwenye menyu ya kushukisha chini ya umbizo la upakuaji, kisha chagua kitufe cha Pakua.

 4. Pindi kitabu kinapokamilisha furushi, chagua chaguo la kupakua faili iliyotayarishwa.

 5. Chagua chaguo la kitufe cha Fungua kwenye Apple Books.

 

Tazama makala kamili ya msaada

Kila kivinjari cha mtandao na programu kinaweza kuhifadhi vitabu vyako kwenye maeneo tofauti. Kwenye kompyuta za Windows, kwanza angalia foolda yako ya vipakuliwa au folda yako ya hati.

Usipoipata faili hapo, pia unaweza kukitafuta kitabu kilichopakuliwa kwenye kompyuta yako. Jina la faili litakuwa maneno machache ya kwanza ya kichwa cha kitabu na mistari itachukua sehemu ya nafasi.

Unaweza kutafuta kwenye kompyuta yako kwa kubofya kitufe cha kuanza na kuchagua tafuta kwenye kompyuta ya Windows (au kwa kubofya Ctrl na Shift kwenye Mac) Ikiwa bado huwezi kukipata kitabu, unakaribishwa uwasiliane na huduma kwa wateja au jaribu kukipakua kitabu tena. 

Tazama makala kamili ya msaada

Ili kupakua faili za BRF kwa kutumia kompyuta au kirekodi madokezo cha Braille, tafadhali fuata hatua za hapo chini. Tafadhali zingatia kuwa hatua hizi hazifanyi kazi unapotumia tableti au simutamba ili kupakua faili za BRF.

 1. Ingia ndani kwenye akaunti yako

 2. Tafuta kitabu kwa kutumia kisanduku cha utafutaji

 3. Chagua kichwa cha kitabu

 4. Chagua BRF kutoka kwenye kisanduku cha kushukisha chini (cha mseto) chenye umbizo la upakuaji, kisha bofya kitufe cha upakuaji

 5. Ukiulizwa kama ungependa Kufungua au Kuhifadhi faili, tafadhali chagua Kuhifadhi, kisha chagua eneo ambapo unaweza kuipata kwa urahisi

Dokezo: Vivinjari vingi vya mtandao vinahifadhi faili kwenye folda ya Vipakuzi kimsingi.

Tazama makala kamili ya msaada

Tafuta Kitabu

Nenda kwenye kisanduku cha Tafuta kwenye sehemu ya juu ya ukurasa wa mwanzo wa maktaba. Andika neno au kirai kinachojumuisha kichwa, mwandishi, au maneno muhimu kutoka kwa kitabu kwenye kisanduku cha utafutaji. Injini yetu ya utafutaji yenye nguvu itaangalia vichwa, majina ya waandishi, na maudhui ya vitabu vyote kwenye maktaba.

Pakua Kitabu

Pindi unapopata kitabu unachokipenda, uko tayari kukipakua na kukisoma!

Soma Kitabu

Njia maarufu zaidi za kusoma vitabu vyetu ni: sauti pekee, kwa braille kwenye kifaa kinachoweza kuonyesha upya cha braille, au kwa sauti iliyolandanishwa na uangazaji wa maneno.

 • Sauti, inayotumiwa na watu vipofu, au kwenye hali ambapo kutazama toleo la maandishi haiwezekani
 • Sauti na Uangazaji wa Maandishi, inasaidia hasa watu wenye tofauti za kujifunza kama vile disleksia au matatizo ya ufuatilizi wa macho
 • Braille, kama vile kifaa kinachoweza kuonyesha upya cha braille, au kikolezwa.
Tazama makala kamili ya msaada

Kuna njia kadhaa za kusikiliza vitabu. Labda uangalie ukurasa wa Vifaa vya Kusoma kwanza ili ujue jinsi unavyoweza kusoma kitabu. 

 • Programu za iOS au Android
  • Ikiwa unatumia kifaa cha kusoma kinachoweza kusoma maandishi ya kitabu, kama vile EasyReader ya Dolphin, unaweza kupata kitabu, kukifungua na kukisikiliza moja kwa moja kwenye kifaa cha kusoma
 • Apple Books
  • Ikiwa umezoea kusoma kwa kutumia Apple Books, basi kipakue kitabu kwenye EPUB na kifungue kwenye Apple Books, ambayo inatoa shughuli ya kusoma kwa nguvu
 • Microsoft Word au Edge Browser:
  • Ikiwa unatumia Word, basi pakua kitabu kwa DOCX na kifungue kwenye Word, ambayo ina chaguo la Kisomaji Tumbukizi ambacho kinasoma kwa nguvu
  • Ikwia unatumia kivinjari cha Edge, basi pakua kitabu kwa EPUB, na kifungue kwenye kivinjari chako, ambacho kina chaguo la Kisomaji Tumbukizi ambacho kinasoma kwa nguvu
 • Vichezaji Sauti (DAISY Sauti au MP3)
  • Ikiwa unatumia kichezaji kinachohitaji faili ya MP3 au DAISY sauti, itabidi utafute na upakue kitabu kutoka kwa tovuti kama faili ya Sauti. Kisha utasongesha faili hadi kwenye kichezaji ili kuifungua na kuisikiliza inapokuwa inachezwa.
  • Idadi kubwa ya vitabu vinavyopatikana kwenye Sauti vinatolewa na injini ya “Maandishi-hadi-Matamshi” (TTS) inayotumia sauti za kompyuta. Injini ya TTS inaweza kuzalisha vitabu vya Kihispani na Kiingereza tu kwa sasa, lakini lugha zaidi zinakuja.
  • Mbali na lugha zaidi za TTS, Maktaba itaongeza vitabu vinavyosimuliwa na binadamu kwenye siku za usoni.
Tazama makala kamili ya msaada

DAISY na BRF ni maumbizo ya dijitali ya nyenzo za walemavu (DAISY inamaanisha Mfumo wa Maelezo ya Walemavu ya Dijitali, na BRF inamaanisha Umbizo Tayari la Braille).

 • Vitabu vilivyoumbizwa kwa DAISY vinaweza kusomwa kama sauti tu au vinaweza kusomwa kwa sauti na uangazaji wa maneno uliolandanishwa kwa wakati sawia. Ikiwa unataka sauti tu, unaweza kuchagua umbizo la upakuaji la DAISY Sauti. Ikiwa ungependa kusikiliza kitabu na kuona maneno yameangaziwa kwenye skrini, chagua umbizo la maandishi ya DAISY au DAISY yenye picha. Utabidi uwe na programu au programu ya simu inayoweza kusoma faili hizi.
 • BRF ni faili ya dijitali ya braille inayoweza kusomwa kwa kifaa kinachoweza kuonyesha upya cha braille na programu zingine za teknolojia ya usaidizi. Unaweza kuchagua kama unataka braille iliyofinywa au ambayo haikufinywa kwenye mapendeleo yako ya akaunti.

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu programu itakayosoma vitabu vyetu, nenda hapa: Vifaa vya Kusoma.

Tazama makala kamili ya msaada