Kila mtu anastahiki haki ya kusoma. Kulingana na makadirio ya Shirika la Afya Ulimwenguni, watu milioni 285 wana matatizo ya kuona, 90% wanaishi kwenye nchi zinazostawi. Idadi kubwa zaidi ya watu wenye ulemavu wa mafunzo na mwili ambao unafanya iwe ngumu kusoma. Vizuizi hizi vinazuia watu wenye ulemavu wasipate elimu, wasiende kazini, na wasishiriki kwenye jamii.

Bookshare® ni maktaba ya vitabu pepe inayorahisisha kusoma. Watu wenye ulemavu wanaweza kusoma kwa sauti, braille, na mbinu zingine za walemavu na wanaweza kubinafsisha huduma kwa njia ambazo ni mwafaka kwao. Kupitia ushirikiano na wachapishi na usaidizi wa wanaojitolea, Bookshare inatoa mkusanyiko mkubwa kabisa ulimwenguni wa vitabu pepe vilivyoko kwenye maumbizo ya walemavu. Uanachama ni bure kwa watu wenye ulemavu unaostahiki.

Bookshare ni jitahada ya Benetech, shirika lisilo la serikali linalokuza jamii kupitia programu za kuboresha jamii. Tangu 2001, Bookshare imesaidia watu wenye ulemavu wasome kwa njia ambazo ni mwafaka kwao. Leo, Bookshare inahudumia malaki ya watu wenye ulemavu kwenye nchi 70.

Unataka kuileta Bookshare kwenye nchi yako? Jifunze kuhusu ushirikiano.